Mwanahabari anayehamasisha kuhusu Ebola ameuawa DR Congo


Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na imelaani mauaji ya mwanahabari anayehamasisha kuhusu Ebola.

Katika taarifa ya pamoja ya wizara ya afya ya nchi hiyo kwa ushirikiano na mashirika ya ya kimataifa yanayohusika na mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola wamelaani vikali mashambulio yaliyofanyika usiku wa Jumamosi katika kijiji cha Lwemba mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.

Wanajeshi wanasema waliwatambua washambuliaji waliovamia nyumba ya Papy Mumbere Mahamba katika kijiji cha Lwebma, eneo la Kaskazini mashariki mwa mkoa wa Ituri, na kumuua, kumjeruhi mke wake na kuteketeza moto nyumba yao.

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana jap mamlaka za nchini humo imeanza uchunguzi kubaini ikiwa ilihusiana na mapambano dhidi ya Ebola.

Washukiwa wawili wanazuiliwa kuhusiana na mauaji hayo

DR Congo inashuhudia mlipuko hatari wa virusi hatari vya Ebola epidemic kwa mara ya pili.

Watu wanaofanya kazi ya kukabiliana na ebola mara kwa mara wanalengwa na nakubdi ya watu wanaopinga juhudi zao.

Mhariri wa BBC, Will Ross anasema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wahudumu kadhaa wa afya wameshambuliwa na watu wanaopinga kampeini ya kukomesha ebola.

Mahambulio hayo yanaaminiwa kuwa kuchochewa na imani ya watu wengi kwamba virusi vya ebola ni njama ya uwongo, hali ambayo imechangia watu kutowaamini watu wanaofanya kazi katika sekta ya afya.

Wataalamu wa afya wakiomba watu kukomesha matambiko ya jadi wakati wa mazishi ili kuhakikisha mtu hajiweki katika hatari ya maambukizi, kwa mfano huzua husababisha chuki.

Watu wengine hata wanafikiria hakuna Ebola na kwamba ni kitu kilichobuniwa na wataalamu wa matibabu ili wapate kazi za mishahara mikubwa.

Nini kilifanyika?

Bw. Mahamba alikuwa akiendesha kipindi cha kuhamasisha watu kuhusu katika kituo cha redio cha kijamii shambulio hilo lilipofanyika.

Profesa Steve Ahuka, mshirikishi wa kitaifa wa wa mapambano dhidi ya Ebola, alithibitisha ripoti kutoka kwa wanajeshi kuwa "mhudumu wa kijamii" aliyekuwa anajihusisha na mapambano dhidi ya Ebola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad