Mwanamitindo wa AFRIKA Kusini Aliyejinunulia Jeneza la Milion 22


Miongoni mwa habari zilizoshtua wengi na kuibua gumzo barani Afrika hivi karibuni ni ya mrembo ambaye ni msanii, mnenguaji, modo, mwigizaji na video queen (muuza sura kwenye video), mwenye umaarufu zaidi mitandaoni (socialite) wa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Zodwa Rebecca Libram Wabantu.

Zodwa mwenye umri wa miaka 34 ambaye ameoa mwanaume na amelipa mahari anajulikana kwa kusababisha matukio huku akiwa na umbo matata (hasa sehemu za nyuma) na kutoona aibu kukaa utupu bila ya kuwa na chupi, ndani kwake nchini Afrika Kusini anamiliki jeneza alilojinunulia la zaidi ya shilingi milioni 22 za Kibongo.

Kwa mujibu wa Zodwa, anajiandaa kwa kifo chake ili atakapokutwa na umauti, basi asiwape watu shida ya kuanza kutafuta jeneza la kumzikia.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, Zodwa alilinunua jeneza hilo miezi kadhaa iliyopita ambapo lilimgharimu kiasi cha shilingi milioni shilingi milioni 22 za Kitanzania.

Tukio hilo liliwashangaza maelfu ya wafuasi wake mitandaoni baada ya kujinunulia jeneza hilo la kifahari kwa ajili ya kujiandaa kwa mazishi yake. Kwa mujibu wa Zodwa, mwenyewe alipata taabu mno wakati wa kuchagua jeneza linalomfaa.

Hata hivyo, Zodwa aliwaeleza wafuasi wake zaidi ya laki tisa mitandaoni kwamba alifanya uamuzi huo kwa sababu hataki kifo chake kiisumbue familia yake na kuanza kuhangaika jinsi itakavyomzika. Katika maelezo yake, Zodwa alisema anataka kila tukio kwenye mazishi yake liendeshwe kwa utaratibu bila tatizo lolote.

“Lazima mtu ujiulize, hivi umejiandaa ipasavyo au unataka familia yako ihangaike wakati umeaga dunia? “Mimi sitaki nikifa watu waseme eti nilikuwa mtu maarufu na pesa nyingi, lakini hakuna pesa ya kugharamia mazishi..,” alisema Zodwa.

Kwa mujibu wa video za tukio hilo, Zodwa anaonekana akijipima kwenye jeneza hilo baada ya kulinunua. Kufuatia tukio hilo, wafuasi wake walionekana kushangazwa huku wengi wakijiuliza ni vipi mrembo huyo haofii kifo wala madhara ya kujipima kwenye jeneza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad