Mwizi mtukutu Nigeria, licha ya kufungwa kwa utapeli, aiba dola Milioni moja na kununua gari la kifahari akiwa gerezani


Hope Olusegun Aroke mfungwa aliyefanya udanganyifu katika mtandao, anafanyiwa uchunguzi nchini Nigeria kwa madai kusuka mpango wa kashfa kubwa ambayo itawagharimu walinzi wa gereza.

 Mfungwa huyo anadaiwa kuiba kiasi cha fedha dola milioni moja za Marekani. Maafisa wa kupambana na rushwa wanasema kuwa bwana Hope Olusegun Aroke alikuwa anatumia mtandao wa kihalifu kufanya udanganyifu akiwa pamoja na washirika wake.

Aroke alishtakiwa mwaka 2012 anatumikia kifungo kwa miaka 24 katika gereza la Kirikiri. Lakini uchunguzi wa awali ulionesha kuwa mtuhumiwa huyo bado anaweza kutumia mtandao hata akiwa gerezani.

Tume ya uchumi na uhalifu wa kifedha nchini Nigeria imetoa tamko linalosema kuwa wamepokea taarifa kutoka kwa wapelelezi kuhusu madai ya uhalifu ambayo bwana Aroke anaendelea kuufanya kwenye mtandao.

Mnamo mwaka 2012, Tume hiyo ilieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Malaysia wakati huo alikuwa anaongoza mtandao wa uhalifu ambao ulikuwa unahusisha mabara mawili.”

Wiki hii tume hiyo imesema kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Aroke alipewa mawasiliano ya mtandao katika simu yake akiwa gerezani.Mtandao

Uhalifu wa mtandaoni

Aroke alikiri katika kituo cha polisi mjini Lagos kuwa ana matatizo ya kiafya na hivyo alipaswa kuondolewa katika eneo hilo na kukaa hotelini ili aweze kukutana na mke wake na watoto wake pamoja na kuhudhuria shughuli za kijamii.

Alikuwa anatumia majina ya kusadikika kama Akinwunmi Sorinmade kufungua akaunti mbili za benki na kununua gari la kifahari wakati akiwa gerezani, tume hiyo iliongeza.

Vilevile amekuwa akitumia kadi ya benki ya mke wake wakati yupo gerezani, ambayo alikuwa huru kuhamisha fedha za ufadhili.”

Maafisa wa kupambana na rushwa wanachunguza kwa nini alilazwa hospitalini na aliwezaje kwenda hotelini na maeneo mengine.

Gereza la ‘Kirikiri Maximum Security’ liko chini ya huduma za hukumu za Nigeria ambazo bado hazijatoa hukumu katika kesi hiyo .

Image result for Hope Olusegun Aroke

Kesi hii imewashangaza raia wengi wa Nigeria, huku wakijiuliza ni namna gani mtuhumiwa aliweza kutumia mtandao akiwa gerezani kwa uhuru kabisa. Wengi wanaamini kuwa Aroke aliweza kupata mwanya huo kwa kutoa rushwa kwa maafisa wa gerezani.

Matapeli wa mtandaoni nchini Nigeria ni matajiri hivyo ni rahisi kwao kuwahonga maafisa wa gerezani ambao wanalipwa kipato kidogo.

Mpaka sasa hakuna aliyesimamishwa kazi kutokana na ulakini huo. Wakala wa kupambana na rushwa ambao walimuweka Aroke gerezani, wameita kitendo hicho kutoeleweka na kuhaidi kufanyiwa uchunguzi .

Haijafahamika kama mamlaka hiyo imefanikiwa kubadili walinzi wake kwa kuwa iko nje ya hukumu iliyotolewa.

Na swali jingine ambalo raia wa Nigeria wanahoji ni kuhusu wafungwa wengi matajiri ambao ni wanasiasa na matapeli wa mtandaoni waliopo gerezani wana uwezo wa kutoa rushwa na kuendelea kufurahia maisha ya kifahari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad