Nancy Sumari Azindua Kitabu cha ‘Haki’


MISS Tanzania mwaka 2005 na pia mjasiriamali, Nancy Sumari, leo Novemba 27, 2019, amefanya ziara ndani ya kampuni ya Global Group alipokuja kutambulisha rasmi kitabu chake kwenye kipindi maalumu kilichorushwa na +255 Global Radio.

Katika mahojiano hayo kwenye kipindi maalumu,  Nancy alisema; “Ninayo furaha kubwa na ya kipekee kutangaza ujio wa kitabu changu cha pili cha watoto!


Meneja wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka,  akiwa na Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari,  wakiwa ndani ya studio ya +255 Global Radio baada ya mahojiano na kisha Nancy kumkabidhi kitabu chake kipya cha ‘Haki’.



“Kitabu hiki, kinachoenda kwa jina la Haki, ni hadithi iliyotungwa kutokana na sheria ya haki za mtoto ya mwaka 2009, ili  kuwasaidia watoto wa Tanzania kuzijua na kuzilinda haki zao.




“Karibuni, pametokea ongezeko la vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za watoto kwa namna nyingi, zikiwemo mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, na mengine mengi yasiyofaa kwa maendeleo na ustawi wa watoto wetu,” aliongeza.




Sumari akimkabidhi kitabu chake kipya cha Haki,  Meneja wa Kampuni ya Global Group Abdallah Mrisho ofisini kwake.



“Kwa kupitia kitabu hiki cha Haki, ninatarajia kumfundisha mtoto wa Tanzania, kuzijua, kuzitambua na kuzilinda haki zake, na vilevile kuibua mjadala kati ya watoto, wazazi, walezi, jamii na taifa kwa ujumla, kuhusu haki za watoto.




“Kwa nafasi yake, anaweza kubeba jukumu la kuzisimamia pamoja na kuwalinda watoto wetu, katika Tanzania tunayoitaka.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad