Waku habari za mchana,kama nilivyojieleza hapo juu,ni kwamba nilibahatika kuoa miaka 10 iliyopita iliyopita, tulipata sakrament ya ndoa takatifu tar.7/5/2011. pia katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 2.
Sasa kilichonifanya nije hapa jukwaani ni taarifa nilizozipata toka kwa jirani yangu ambae amenithibitishia kuwa mke wangu anatembea na mtu ambae pia ni jirani yetu kabisa. mke wangu huwa anashinda nyumbani akijishughulisha biashara ya kiduka tulichokifungua karibia mwaka sasa. pia mimi huwa nashinda kibaruani kwangu ambapo mara nyingi huwa nachelewa kurudi nyumbani kutokana na kabiashara kangu kanakonipatia riziki.
Huyu jirangu kanijulisha huwa wanatoka majira ya saa 1 jioni na kurudi sa 2:30 jioni kabla mimi sijarudi. baada ya kupata tarifa hizi nilijaribu kufanya uchunguzi na nimeanza kuona kuna ukweli juu ya jambo hili. juzi ilipofika saa 1:30 jioni nilimpigia simu kumuulizia jambo fulani nikasikia anaongea taratibu tofauti na siku nyingine, nikamuuliza umeshafunga duka? akanijibu ndio, Nikamuuliza mbona mapema akasema kuna mkanda nimeupenda nauangalia..nikakata simu nikampigia yule jirani kumuuliza kama mke wangu yupo nyumbani akasema hayupo na ametoka na jamaa kama kawaida yake, kama huamini uje uone. nilitamani kwenda lakini nilishindwa kujua ni uamuzi gani nichukue kwa sababu, kwanza sikujua wamekwenda Guest gani
Huyo jamaa anausafiri hivyo wanauwezekano wa kwenda nje ya mji kidogo, nilijikaza sikumuuliza wala kumwonyesha dalili zozote za kufahamu mambo hayo machafu anayoyafanya mke wangu
Hivyo naombeni ushauri wenu pindi nikiwafumania au kuwahi kurudi home na kumkosa mke wangu wakati amenijulisha yupo home..Naombeni ushauri wenu ni uamuzi gani naweza kuchukua ukawa sahihi.
muonye aaache huo uchafu mpe nafasi ingine ila mtenge kitanda hata mwezi mmoja ajifunze usimpige wala nini
ReplyDeleteKabla ya kumfumania, hebu jiulize UNA'MOYO?? Kama huna'moyo usijisumbue kufumania, utakufa bure, we mpotezee ila mshauri atumie kinga, na wewe tafuta mchepuko iwe ngoma'droo......siku mkichoka kuchepuka, mtakaa kama kamati......
ReplyDeleteIla mimi mwenyewe binafsi ningetimua maana siku hizi magonjwa mengi.... Sasa wewe ndugu unathamini biashara kuliko kitumbua chako inawezekana humkanyagi vizuri kwa sababu ya biashara sasa wewe komaa na biashara acha watu wakanyage kitumbua
ReplyDeletekwa upande wangu siku zote huwa naamini kuwa mambo ya mahusiano huwezi kumshauri mtu au kuomba ushauri kwa mtu......maamuzi unafanya mwenyewe kutegemeana na jinsi unavyoweza kuli andle jambo husika na tabia za mtu husika..........but kama ili jambo lingekuwa kwenye maamuzi yangu ningetafuata ushahidi na kumwacha huyo mwanamke.
ReplyDelete