Ndege Nyingine ya Tanzania yakamatwa Canada

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi, amesema kuwa kumekuwa na hujuma kubwa zinazofanywa na mabeberu za kurudisha nyuma juhudi na maendeleo ya nchi mara baada ya kuishikilia kwa mara nyingine tena Ndege aina ya Bombadier Q400, nchini Canada.


Hayo ameyabainisha leo Novemba 23, 2019, Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa mara baada ya ndege hiyo kukamatwa alimuita Balozi wa Canada hapa nchini na kumueleza ni kwa namna gani Serikali ya Tanzania, imekuwa ikikasirishwa na vitendo vya ndege zake kukamtwa nchini humo kila ikifikia hatua ya kurudi Tanzania, hali inayoashiria kudidimiza juhudi na maendeleo ya nchi.

"Juzi limetokea jambo la kusikitisha ambalo ni vyema watanzania pia walielewe jinsi ambavyo hujuma za kibeberu zikifanyika kurudisha kasi ya maendeleo, tena kwa mara ya tatu Ndege ambayo ilitakiwa kufika Tanzania imekamatwa tena Canada na kesi ipo mahakamani na aliyefanya hivyo ni mtu yuleyule aliyekamata Ndege yetu Afrika Kusini, tukaenda mahakamani tukamshinda sasa amekimbilia Canada na amekamata Ndege yetu ya Bombadier Q400". amesema Waziri Kabudi.

Aidha Profesa Kabudi amemshauri Rais Magufuli, kama ikiwezekamna waache kununua ndege nchini Canada kwakuwa mara nyingi Ndege zimekuwa zikikamatwa nchini humo, lakini zinazotoka Marekani zinafika salama .

"Jana nimemuita Balozi wa Canada na alifika Dodoma na nimemuambia kinagaubaga na bila tashwishwi kwamba hatufurahishwi kabisa kwa tabia na vitendo hivi vya kila Ndege yetu inapotakiwa kuondoka Canada kurudi Tanzania inakamatwa na kwamaana hiyo tunafikiri Mhe Rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu hivi sio wao pekee wanatengeneza Ndege, hatukufanya makosa kwenda kununua kwao hata Brazil wanatengeneza ndege" amesema Waziri Kabudi.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa tayari hatua zote za kimahakama zimekwishachukuliwa ili kuweza kuikomboa Ndege hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad