Nimeenda Sana kwa Mganga na Nimewaumiza Sana Watu Wakati Mwingine Nasema Nilistahili Kupitia Niliyoyapitia- Muna Love

SIKU zote ukweli humweka mtu huru! Hilo ndilo linalojiri kwa mwigizaji wa sinema za Kibongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ ambaye ameamua kuweka wazi kuwa amekwenda sana kwa waganga wa kienyeji (sangoma).  Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, Muna anasema hizo ndizo zilikuwa zake kabla ya kumpa Mungu maisha yake.

“Nimepitia mambo mengi sana katika maisha yangu, ukiniuliza kama niliwahi kwenda kwa waganga nitakumbia sana tu, unajua siku zote ukweli unakuweka huru na nimekiri hivyo na roho yangu imekuwa nyeupe,” alisema Muna ambaye sasa anamtumikia Mungu kwa namna tofauti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad