Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya 29 kabla ya Fahad Bayo kutupia la pili dakika ya 66 na kuiwezesha Cranes kukaa kileleni mwa Kundi B ikiwa na pointi nne sawa na Burkina Faso ambayo siku hiyo nayo iliichapa Sudan Kusini kwa bao 1-0.
Katika kundi hilo upinzani mkali unaonekana kuwa kwa timu tatu, kutokana na Malawi kushika
nafasi ya tatu ikiwa na alama zake tatu wakati huu Sudan Kusini ikiburuza mkia bila pointi.
Akizungumza na BBC Redio, Okwi alisema mchezo huo haukuwa rahisi kwao hata kidogo licha ya
kuibuka na ushindi huo, lakini kikubwa wanashukuru kuweza kushinda.
"Kwanza nashukuru tumepata ushindi, Malawi ilikuwa inaonekana nyepesi magazetini, lakini ni timu
ngumu na mimi nashukuru nimepata bao ambalo limesaidia timu yangu kuibuka na ushindi,"
alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba.
Wageni hao, Malawi ambao waliichapa Sudan Kusini bao 1-0 katika mechi ya kwanza, walijaribu
kucheza pasi nzuri lakini ilikuwa kazi kuweza kuipenya safu ya ulinzi ya Uganda ambayo pia