PAUL Makonda Aagiza MALL Zote Dar Kufungwa Saa 6:00 usiku


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa rai kwa wamiliki wote wa maduka makubwa 'Shopping Mall' ndani ya Jiji hilo, kuhakikisha wanaanza kufunga kuanzia saa 6:00 usiku, kwakuwa ulinzi na usalama upo wa kutosha.


Makonda ametoa kauli hiyo kuelekea Mkutano Mkuu wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka nchi 29 za Afrika na nchi 5 za Nordic, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuufungua mkutano huo siku ya Novemba 8, 2019.

"Nitoe rai kwa Malls zote kama vile Mlimani City na zingine, sisi kiusalama tuko vizuri, tungependa hili juma na wao waongeze muda wa kufanya biashara mpaka saa 6 usiku, tunataka hao wageni wetu wakimaliza mikutano yao pale Mwalimu Nyerere, wawe na uwezo wa kwenda pale Mlimani City wakanunua bidhaa mbalimbali" amesema Makonda.

Aidha Makonda amewapa fursa wafanyabiashara wa vinyago, uchoraji na utengenezaji wa vifaa vya utamaduni ndani ya Jiji hilo, kuanzia kesho Novemba 7 kuanza kuonesha sanaa zao katika barabara ya Chuo cha IFM ili watumie fursa ya ugeni huo kufanya biashara na kujitangaza kimataifa, kama walivyofanya kipindi cha mkutano wa SADC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad