Polisi Nigeria imewaokoa zaidi ya watu 250 waliokuwa wameshikiliwa katika msikiti

Polisi nchini Nigeria imewaokoa watu 259 kutoka katika kituo kisichokubalika kisheria kilichopo ndani ya msikiti katika mji wa Ibadan, uliopo katika jimbo la kusini magharibi mwa nchi hiyo la Oyo, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.



Wengi miongoni mwa waliookolewa katika uvamizi wa polisi walikuwa wamefungwa kwa minyororo katika eneo la msikiti, amesema msemaji wa Polisi Gbenga Fadeyi.

Katika kipindi cha uliopita, zaidi ya watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vituo vya kidini ambako mara kwa mara watu wamekuwa wakishikiliwa katika hali mbaya.


Image captionPolisi inasema baadhi ya waliookolewa katika msikiti huo walikuwa wameishi kwenye kituo hicho kwa miaka kadhaa
Wazazi wamekuwa wakiwatuma watoto wanaowasumbua kitabia na vijana wanaoaminiwa kuwa na uraibu wa madawa ya kulevya au wale waliopatikana na makosa madogo katika vituo vya Koran vya kurekebisha tabia.

Lakini maafisa wamevifananisha vituo hivyo na vituo vya ukatili ambapo watu wanafungwa minyororo , kufungwa pamoja na kufanyiwa dhuluma.

Waliotekwa waliachiliwa Jumatatu jioni baada ya polisi kupewa taarifa na kijana mwenye umri wa maika 17 ambaye alikuwa ametoroka kutoka katika mahabusu nyingine katika eneo hilo.

Mmiliki wa mahabusu hiyo na watu wengine wanane wamekamatwa , limeripoti gazeti la Punch nchini humo.

Wanawake walikuwa ni miongoni mwa watu waliookolewa mwezi uliopita kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia cha kiislamu nchini NigeriaWanawake walikuwa ni miongoni mwa watu waliookolewa mwezi uliopita kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia cha kiislamu nchini Nigeria mwezi Oktoba mwaka huu
Kamishna wa polisi wa jimbo hilo Bwana Shina Olukolu alinukuliwa akisema kwamba baadhi ya waathriwa wa utekaji huo wamesema wamekuwa wakishikiliwa kwa miaka kadhaa.

Hali katika msikiti huo ilikuwa ni mbaya kwa binadamu kuishi na baadhi ya vifo vya waathirika vilivyotokea havikuripotiwa, alinukuliwa akisema.

Huu ni mojawapo ya uvamizi wa wa hivi karibuni wa vituo vinavyoitwa ”vituo vya kiurekebisha tabia” nchini Nigeria ambamo watu wanashikiliwa katika hali mbaya mkiwemo kufungwa na minyororo.

Wengi husajiliwa kwenye taasisi hizo na ndugu zao ili kupata usaidizi wa kiroho na kurekebisha tabia kwa wanaotumia madawa ya kulevya.

watoto
Mwezi uliopita polisi nchini Nigeria waligundua zaidi ya vijana 70 wakiwa wamefungwa katika shule binafsi ya kiislamu kaskazini mwa Nigeria.

Mamia ya vijana wametoroka katika shule mbalimbali za dini ya kiislamu katika siku za hivi karibuni.

Shule za bweni za kiislamu zinazojulikana kama Almajiris ni maarufu sana kwa waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad