Polisi wapekua nyumbani kwa Idriss


Kufuatia suala la Idriss kushikiliwa na Polisi kwa kuvunja sheria ya mtandaoni kifungu namba 15 na 16 ambavyo vinaeleza kuhusu kutengeneza taswira ya kuigiza kwa kutumia kompyuta pamoja na kusambaza taarifa zenye uongo ndani yake.

Polisi wanadaiwa kufika nyumbani kwa Idriss Sultan na kufanya upekuzi, hii inatokana na ishu yake inayomkabili ya kuhariri picha ya Rais katika ukurasa wake wa Instagram.

”Ni kweli polisi walimuhoji Idriss Sultan kuanzia saa 5 pale central mpaka saa tisa wakaondoka nae, tunapoongea sasa hivi wapo nyumbani kwake wanamaliza upekuzi halafu tunarudi tena kituoni kwa ajili ya dhamana”, amesema Benedict Ishabakaki ambaye ni wakili wake.

Hayo yote yanajiri kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, aliyemtaka ajisalimisha kituo cha polisi kufuatia baadhi ya post alizoweka katika mtandao wa Instagrama baada ya kujivalisha sura ya Magufuli katika siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akimtakia heri ya kuzaliwa.

Makonda alitoa agizo hilo kupitia ukurasa wake wa instagrama ambapo aliandika kuwa.

Naona mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha polisi uwambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako,”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad