Pompeo aadhimisha miaka 30 kuangushwa ukuta wa Berlin kwa lawama


Katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin yaliyofanyika hapo jana, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo amezishutumu nchi za Urusi na China kwa kuongoza kwa kutumia nguvu.

Shutuma hizo amezitoa alipokutana na viongozi wa Ujerumani katika ziara yake ya kuenzi siku ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.

Pompeo amesema Marekani inakubali kutokea kwa kasoro baada ya kuangushwa kwa ukuta huo na kusema vikosi vya kijeshi viliondolewa chini ya dhana kuwa watu sasa wapo huru, ila anafikiri hilo lilikuwa kosa.

Amesema hii leo Urusi inaongozwa na waliyekuwa afisa wa shirika la usalama la uliokuwa Muungano wa Kisovieti, KGB mjini Dresden ambaye huvamia majirani zake na kuwaua wapinzani wake wa kisiasa.

Hata hivyo hakusita kutupia lawama uongozi wa China kwa jinsi ulivyowalenga wanaharakati wa Xinjiang, HonhKong na wale walio uhamishoni nchini ujerumani na katika bara la Ulaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad