Prof. Lipumba Atuma Ombi kwa Rais Magufuli



Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) amemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kile alichokidai ni kuepusha vurugu na matatizo kwenye uchaguzi huo.

Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajia kufanyika Novemba 24, 2019.

"Kuepusha suala la vurugu kwenye Uchaguzi huu, naomba Rais Magufuli aingilie kati suala hili na wagombea walioenguliwa wapewe nafasi ya kuteuliwa kugombea".

Profesa Lipumba ameendelea kwa kusema,"Kitendo cha kuwanyima fomu wagombea wa upinzani sio tu halina tija kwenye ukuaji wa Demokrasia, pia ni matumizi mabaya na hela za umma, huwezi ukafanya semina, kuchapisha nyaraka mbalimbali huku ukijua hakuna uchaguzi bali wagombea wanapita bila kupingwa".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad