Raia wa Marekani anayeshukiwa kuwa mfuasi wa IS akwama 'mpaka wa Uturuki na Ugiriki'


Mtu anayeshukiwa kuwa mpiganaji wa Jihad akiwa amesimama kati ya mpaka wa Uturuki na Ugiriki
Raia wa Marekani aliyeshukiwa kuwa mwanamgambo wa Isalamic State amekwama katika mpaka wa Ugiriki na Uturuki, baada ya Uturuki kumfukuza.

Mshukiwa huyo alisafirishwa siku ya Jumatatu wakati Uturuki ilipoanzisha mpango wa kuwarejesha wapiganaji wa jihadi waliokuwa wakishikiliwa kwenye magereza.

Polisi nchini Ugiriki wamesema walimkatalia kuingia alipojaribu kuvuka mpaka karibu na mji wa Kastanies nchini Ugiriki.

Mwanaume huyo anaripotiwa kukwama kwa siku mbili katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

Ametajwa na Shirika la habari na Uturuki kuwa Muhammed Darwis B na kusema kudaiwa kuwa raia wa Marekani mwenye asili ya Jordan.

Afisa wa Uturuki ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa alikataa kurudishwa Marekani na badala yake aliomba apelekwe Ugiriki.

Mustakabali wa wapiganaji wa IS limekuwa swali muhimu tangu kudhibitiwa kwa kundi hilo kwenye maeneo waliokuwa wakidhibiti nchini Syria na Iraq.

Raisi a Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ameeleza kuwa wanamgambi 2,500 wako gerezani nchini Uturuki.

Kuna mafanikio baada ya vita dhidi ya IS?
Zaidi ya nchi 70 ziliungana kupambana na kuangusha utawala wa jihadi nchini Iraq na Syria. Lakini kwa kampeni nyingine katika eneo la Mashariki ya kati, walishindwa kupanga ipasavyo jinsi ya kuyakabili matokeo.

Kutokana na mapigano ya mwisho dhidi ya IS katika mji wa Baghuz nchini Syria mwezi Machi, maelfu ya wapiganaji wa IS na wategemezi wao waliposhikiliwa kwenye makambi. Uturuki ambayo imekuwa ikiwakamata wafuasi wa IS kwa miaka kadhaa, sasa ina takribani wafuasi 2,000 wa IS.

Uturuki, Iraq na mamlaka za kikurdi wote wanataka Ulaya na nchi za magharibi kuharakisha kuwachukua raia wao lakini mpaka sasa serikali zimesita kufanya hivyo, moja ya sababu ni hofu ya kushindwa kuwashtaki.

Uturuki imemsafirisha nani mwingine?
Wizara ya mambo ya ndani imesema pia imerudisha raia wa Denmark mtu anayedaiwa kuwa mfuasi wa IS siku ya Jumatatu. Mamlaka ya Denmark imesema raia wake alikamatwa alipowasili mjini Copenhagen.

Ujerumani imesema mmoja wa raia wake pia alifukuzwa.

Uturuki imesema washukiwa 20 wenye asili ya Ulaya, wakiwemo raia 11 wa Uaransa, wawili wa Ireland na kadhaa wa Ujerumani, wako katika mchakato wa kurudishwa kwenye nchi zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad