Rais Magufuli akutana na Bosi wa TDB Afrika Mashariki na Kati


Rais Dkt. John Magufuli hapo jana amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Admassu Tadesse, Ikulu jijini Dodoma.

Tadesse akiwa ameambatana na ujumbe wake aliwasili Uwanja wa Ndege wa jijini Dodoma na kulakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge.

Akizungumza muda mfupi baada kumaliza mazungumzo yake na Rais Magufuli, Tadesse amesema TDB itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania na kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi yake mbalimbali ya maendeleo nchini.

Dkt. Mpango amesema TDB imekuwa moja ya Benki kinara ambayo imekuwa ikitoa mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya maendeleo.


Aidha, Tadesse akiwa nchini anatarajiwa pia kutembelea maeneo mbalimbali sambamba na kujionea miradi ya maendeleo inayotelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa na miradi mingine ambayo mkopo kutoka (TDB) utaelekezwa.

Tadesse amesifu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Benki hiyo ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad