Rais Magufuli: Watu wanataka kusajili laini zao lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa


Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma

“Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho” amesema.

"Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima".

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.

“Wengine wanalalamikia bei ya mahindi kupanda, nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha,” amesema Rais Magufuli.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad