Rais wa Bolivia Ajiuzulu, Atangaza Uchaguzi Mpya

Rais wa Bolivia ajiuzulu, Atangaza uchaguzi Mpya
Rais wa Bolivia aliyeongoza kwa kipindi kirefu zaidi, 2006-2019 ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kutokana na vurugu zinazoendea nchini humo.

Hayo yamejiri baada ya kukubaliana na matokeo ya uchunguzi uliokuwa unafanywa na wachunguzi wa kimataifa juu ya mwenendo wa uchaguzi uliopita na kumfanya asalie madarakani.

Wachunguzi hao walitengua matokeo yaliyomtangaza Morales mshindi wakisema kulikuwa na udanganyifu katika upigaji wa kura mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.

Licha ya kujiuzulu, Morales ametangaza nia ya kuitisha uchaguzi mpya na kuvunja tume ya uchaguzi ambayo ilikuwa awali.

Amenukuliwa akisema kuwa ameamua kuitisha uchaguzi mwingine ili Wananchi wa Bolivia waweze kuchagua Serikali mpya kwa njia ya Kidemokrasia.

Kwa wiki kadhaa sasa nchi ya Bilivia imeshuhudia machafuko na ghasia dhidi ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 20, ambapo watu watatu wameuawa na zaidi ya 300 wamejeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi uliopita yalimpa ushindi Morales kwa asilimia 10 zaidi dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa na kupelekea upande wa upunzani kuishutumu Serikali kwa udanganyifu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad