RC Makonda Apiga Marufuku Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza Kupewa Mradi Dar es Salaam, Ni baada ya Kampuni Hiyo Kuzidisha "Ubabaishaji"
1
November 03, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Novemba 02 amewataka TANROAD kuhakikisha Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza haipatiwi mradi wowote wa ujenzi ndani ya mkoa huo baada ya kampuni hiyo kuendelea kusuasua kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Kivule licha ya Kupewa fedha za ujenzi.
RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo akiwa kwenye barabara ya Kivule yenye urefu wa Km 3.2 ameshuhudia Mkandarasi huyo akiwa na uhaba wa Vifaa licha ya kudanganya kwenye mikataba kuwa anavyo vifaa vya kutosha ili apatiwe tenda jambo lililopelekea mradi kuchukuwa muda mrefu bila kukamilika.
Aidha RC Makonda amesema mradi huo ndio utakuwa wa mwisho kwenye mkoa huo huku akizionya bodi za manunuzi zinazotoa tenda Kwa kuendekeza Rushwa na kujuana jambo linalowafanya kushindwa kumuonya mkandarasi kwakuwa tayari wamefungwa midomo Kwa rushwa.
Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao kwa sasa upo kwenye hatua ya kufunika gorofa ya kwanza huku akieleza kuwa anaamini ujenzi utakabidhiwa Mwezi Disemba.
Katika hatua nyingine RC Makonda ametembelea ujenzi wa Mto Sinza na Mto Ng'ombe wenye urefu wa Km 7.5 ambao baada ya kuwakamata wakandarasi hatimae ujenzi sasa umeanza huku akimtaka mkandarasi wa kampuni hiyo kumaliza mradi kwa wakati.
Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya NAMIS Corporate LTD inayojenga Soko la Tandale kukamilisha ujenzi huo haraka ili wafanyabiashara wauze bidhaa katika sehemu nzuri.
Itakumbukwa kuwa October 24 RC Makonda aliagiza kukamatwa Kwa wakandarasi wa kampuni ya CHICO na Nyanza baada ya kampuni hizo kusuasua kwenye miradi Kwa muda mrefu na hatimae sasa wakandarasi wameingia kazini
Tags
Tatizo la makandarasi ni sugu na linakera na halipaswi kuendea kuishi ndani ya Tanzania. Tumechoka. Sasa serikali ichukue hatua sahihi kulitokomeza. Kama kandarasi haogopi hata miradi ya serikali, je hali ipoje kwa miradi ya watu binafsi? Ni kawaida sana kuona au kusikia fundi au kandarasi aliyepewa kujenga nyumba ya mtu fulani hakutimiza wajibu wake ndani ya wakati au kwa kiwango kitakiwacho. Je hali hii tuiache iendelee kuishi ndani ya taifa letu na kuwa moja ya tamaduni zetu. Hilo lipo kwenye mikono yetu kuamua. Enough is enough
ReplyDelete