Sakata la Mbelgiji Simba Lafikia patamu


Mvurugano! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia filamu ya Kocha wa Simba, Patrick Aussems na mabosi wa timu hiyo kuonyesha kuvimbishiana ndani ya klabu hiyo. Juzi Alhamisi, Aussems, raia wa Ubelgiji, alikutana na kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kupewa barua ya kusimamishwa kazi kwa muda wa siku tano na kutakiwa ajitetee kabla ya kufanyika kwa maamuzi mazito.



Ikumbukwe kuwa Aussems alikumbana na balaa hilo baada ya kudaiwa kuondoka nchini kinyemela na kwenda Afrika Kusini ambako inasemekana alienda kumalizana na timu ya Polokwane City ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini humo.



Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Mwekezaji Mkuu wa Simba, Mohammed  Dewji ‘Mo’, kikiwa chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Simba, Moses Kaluwa, inadaiwa kuwa Aussems alibanwa katika mambo matatu ambayo alitakiwa ayatolee ufafanuzi wa kina kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.



Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumamosi limezipata zimedai kuwa, jambo la kwanza ambalo Aussems alitakiwa kulitolea ufafanuzi lilikuwa ni juu ya kitendo chake cha kuondoka nchini kinyemela na kwenda zake Sauz.



“Viongozi walitaka kujua kuhusiana na hilo ambapo kocha aliwaambia kuwa aliondoka nchini baada ya kupata matatizo ya kifamilia ambayo alitakiwa kwenda kuyatatua haraka iwezekanavyo.



“Lakini pia kabla ya kuondoka alimwandikia barua kwa njia ya email mtendaji mkuu wa klabu hiyo raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingisa ambaye kwenye kikao hicho cha jana (juzi) hakuwepo huku akionyesha ushahidi wa email hiyo.



Jambo la pili “Jambo la pili ambalo uongozi huo ulitaka kulijua ni kuhusiana na kitendo chake cha kukaidi wito wa Senzo aliompatia baada ya kurudi

nchini akitokea Sauz. “Alichowaambia viongozi hao ni kwamba siku ambayo alitakiwa kukutana na Senzo alinyeshewa na mvua wakati alipokuwa mazoezini akifundisha timu hiyo kwa hiyo asingeweza kwenda kuonana naye wakati huo akiwa ameloa.



“Alisema kuwa aliwasiliana na Senzo na kumwambia kuhusiana na hilo, hivyo akawa anasubiri wito mwingine kutoka kwa kiongozi wake huyo lakini hakufanya hivyo mpaka alipopewa barua ya kusimamishwa. JaMaBo la tatu “Aussems pia aliulizwa ishu ya kwenda Mbuga ya Serengeti kula bata na mkewe wakati ligi kuu ikiendelea.



“Baada ya kutakiwa kutoa maelezo juu ya hilo alisema kuwa, wakati anaenda Serengeti, timu hiyo ilikuwa katika mapumziko ya siku tatu, hivyo akatumia muda huo kwenda kupumzika na mkewe kwa hiyo hakuona haja ya kubakia Dar wakati timu ipo katika mapumziko hayo,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza: “Baada ya kumuuliza mambo hayo na kuwapatia majibu, kamati hiyo ilimwambia kuwa kazi yao ilikuwa ni kumhoji kuhusiana na mambo hayo, hivyo maamuzi yote ya nini kitafuatia baada ya zoezi hilo atayapata kutoka kwa CEO.”



AWASILIANA NA SENZO

“Hata hivyo leo asubuhi (jana) aliwasiliana na Senzo ili kujua kama anaweza kuendelea na majukumu yake ya kuifundisha timu hiyo, lakini kiongozi huyo alimkatalia na kumwambia asubiri kwanza mpaka atakapopata barua.” Alipotafutwa Senzo ili azungumzie ishu hiyo simu yake iliita tu bila kupokelewa.



AUSSEMS AIBUKIA TWITTER

Kupitia mtandao wa Kijamii wa Twitter, Aussems amekiri kusimamishwa na uongozi wa timu hiyo kutekeleza majukumu yake huku akishindwa kuweka wazi sababu ya kusimamishwa kwake. Aussems aliandika: “Kwanza nawashukuru wote ambao mnanipa sapoti kwa jumbe mnazonitumia, nimezuiwa na bodi kwa kuwa bado nimesimamishwa kufanya kazi yangu, matarajio yangu ni kuendelea kuwapa soka la kuvutia ikiwa ni ushindi pamoja na makombe kwa mashabiki.”- wa Simba.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad