Serikali yaonya Vyombo vya Habari kuhusu hili


Serikali imesema itavichukulia hatua kali za kisheria vyombo vya habari ambavyo vinatoa taarifa zinazosigina misingi ya kitaaluma ikiwemo kutojiridhisha ikiwa taarifa inayotolewa ni ya kweli.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dk. Hassan Abas ametoa onyo hilo jana Novemba 27, 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Dk. Hassan Abas amesema kuwa siku za karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya vyombo vya habari nchini kushabikia na kutumika kama mawakala wa kusambaza habari za uongo, uzushi na propaganda dhidi ya nchi kwa mashirika ya kimataifa au wawakilishi wa mataifa ya nje.

"Bahati mbaya katika habari hizo misingi ya taaluma ya habari husiginwa hasa kanuni ya kujiridhisha na ukweli wa tuhuma husika. Kwa sababu hiyo;

"Serikali imeelekeza vya kutosha, imeonya vya kutosha na imesamehe vya kutosha. Sasa tutachukua hatua kali za kisheria." ameeleza msemaji huyo mkuu wa serikali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad