Dar es Salaam. Mkurugenzi Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema sifa ya mhudumu wa ndege ni elimu na vigezo vinavyokubalika kimataifa na kitaifa.
Amesema mvuto kwa wahudumu wa ndege za shirika hilo sio lazima, haupo kwenye viwango na kanuni, “ingekuwa sheria zetu zinataka wanaotembea kwa maringo tungewachukua lakini na huduma nazo zingetolewa kwa maringo.”
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 9, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari akitoa ufafanuzi wa kauli ya mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima ambaye siku mbili zilizopita bungeni mjini Dodoma alisema wahudumu wa shirika hilo hawana mvuto kwa wateja.
Amesema lengo la mkutano huo na wanahabari ni kutoa elimu kwa wananchi wasiokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sifa za wahudumu wa ndege.
"Kusema kuwa wahudumu ni wafupi si kweli. Waliopo wana urefu wa futi 5.2 na wanaweza kuyafikia maeneo yote (ndani ya ndege), hilo la ufupi sijui limetoka wapi. Hata kusema ni watu wazima sio kweli wanaanzia umri wa miaka 18 hadi 48.”
"Siyo kama hatutaki kupokea maoni ya wadau lakini yanapotolewa kinyume tunapaswa kutoa elimu ili kuondoa mkanganyiko," amesema Matindi, akibainisha kuwa kinachotakiwa ni huduma stahiki.
Na akiwepo mwenye sifa hizo halafu pia mwembamba mrefu kama ilivyo kwa mashirika mengine ya ndege kote ulimwenguni je?
ReplyDeleteMtu wa futi 5 na inchi mbili, ni mifupi. Angalau ingefanya kuanzia futi 5 inch 5 na kuendea. Asiwe round. Tusiyapuuzie hayo na wala si kashifa kusema hivyo kwani watu wa kazi hizo huwa na muonekano maalum naamini ni part ya ushindani katika biashara hiyo. Pamoja na vigezo vyote hivyo. Uniform zao hupendeza zikiwa ndani ya size maalum. Ila asifutwe kazi ambaye ana sifa na pia mfupi au hajanyooka, bali apewe kazi nyingine kama vile kwenye desk na kadhalika. Hilo ni la kufanyia kazi watafutwe air hostess wenye sifa zote, tafadhali.
ReplyDeleteNdugu matindi, kwa kazi hii vinatakiwa vyote viwili huduma na muonekano, si tunaona kwenye TV wahudumu wa Carter, tunawaona kwa macho yetu wahudumu wa klm, emirates, ba nk. Kama warembo wapo na wanavigezo , basi hiyo pia ni jambo jema kuwapa kozi ya kuwafanya wafiti kazi na wapewe mtihani na wakipass basi wachukuliwe. kazi zingine huwa zinazungumza zenyewe na wala hazihitaji wa kuzitetea. Mashirika hayo makubwa huwaajiri wahudumu hata nje ya nchi. Hilo lishughulikiwe kwa makini.
ReplyDeleteHuo hapo chini ni mfano tu
ReplyDeletewww.google.co.uk/search?source=hp&ei=N4bHXbjnMYaTlwSiw4LYAg&q=Factors+required+to+be+an+airhostess&oq=Factors+required+to+be+an+airhostess&gs_l=mobile-gws-wiz-hp.3...89915.142523..142541...2.0..2.3513.14773.0j22j2j1j0j2j1j9-3......0....1.......8..41j41i131i275j0i131j46i131j0j46j0i22i30j33i22i29i30j33i160j33i21..19%3A11.mDJIEyvjP9w