Siku 20 Baada ya Uchaguzi, Rais Ajiuzulu, Atanganza Uchaguzi Mpya


RAIS wa Bolivia, Evo Morales,  amejiuzulu kufuatia maandamano ya kumshinikiza kufanya hivyo yaliyosambaa nchi nzima na kuungwa mkono na polisi na jeshi, kutokana na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 20, mwaka huu.



Wachunguzi wa kimataifa waliokuwa wakichunguza uchaguzi ulifanyika nchini humo jana walitengua matokeo yaliyomtangaza Morales mshindi wakisema kulikuwa na udanganyifu katika upigaji kura hizo.



Morales ambaye amedumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2006, alikubaliana na uchunguzi huo na kutangaza uchaguzi mwingine mpya ikiwa ni baada ya kuivunja tume ya uchaguzi ya nchi hiyo huku akiwataka wananchi kuacha vurugu na kuharibu mali.



Amenukuliwa akisema  ameamua kuitisha uchaguzi mwengine ili wananchi wa Bolivia waweze kuchagua serikali mpya kwa njia ya kidemokrasia.



Kwa wiki kadhaa Bolivia imeshuhudia machafuko na ghasia dhidi ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 20 ambapo watu watatu wameuawa na zaidi ya 300 kujeruhiwa.



Matokeo ya uchaguzi uliopita yalimpa ushindi Morales kwa asilimia 10 dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa na kusababisha upande wa upinzani kuishutumu serikali kwa udanganyifu.

YOU MAY LIKEMgid

Her 50 Kg Weight Loss Took Weeks With 1 Simple Solution

Drink 1 Glass Every Night And Watch Your Fat Burn Like Crazy

You Won't Believe The Results That People Are Getting From This

8 Cute Animals That Are Actually Deadly Machines

Love Lasts Longer When You Break These 6 Rules

Are You The Kind Of Woman He's Looking For?

TOA COMMENT

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad