Simba Vs Prison, Twitter ya Simba yazua Mjadala


Kuelekea mchezo wa leo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prison, utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ukurasa wa Twitter wa klabu ya Simba umezua mjadala miongoni mwa mashabiki.


Wachezaji wa Simba, kutoka kushoto ni Clatous Chama, MIraji Athumani na Hassan Dilunga.

Simba ambayo sasa ina alama 21 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu, imezipa majina ya wachezaji alama hizo kutokana na namba za jezi zao.

Alama hizo zimeitwa Miraji Athuman kutokana na mchezaji huyo kuvaa jezi namba 21.

Alama Miraji (2⃣1⃣) tukiwa kileleni mwa msimamo wa #VPL. Kesho tukiwashughulikia vizuri Prisons tutafikisha alama Dilunga (2⃣4⃣ )  #NguvuMoja pic.twitter.com/vUvLvu8ErJ

— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) November 6, 2019

Aidha Simba imeonesha matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo baada ya kuzipa jina alama 24 watakazofikisha endapo watashinda. Alama hizo wameweka wazi kuwa wataziita alama Hassan Dilunga kutokana na nyota huyo kuvaa jezi namba 24.

Alama Miraji (2⃣1⃣) tukiwa kileleni mwa msimamo wa #VPL. Kesho tukiwashughulikia vizuri Prisons tutafikisha alama Dilunga (2⃣4⃣ )  #NguvuMoja pic.twitter.com/vUvLvu8ErJ

— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) November 6, 2019

Mashabiki nao hawakuwa mbali, wameungana na ukurasa huo wa Simba huku wengine wakitaja namba kama 17 ya Clatous Chama itumike wakifikisha alama 27.

Tukishinda tena game itakayo fuata tutakuwa na alama @ClatousC 27

— senyael siphael pallangyo (@Senyaelsiphael) November 6, 2019

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad