Simon Msuva Aigomea Teknolojia ya AVR

Wakati Morocco ikiwa nchi ya kwanza kutumia Teknolojia ya Video ya Kumsaidia Refa (VAR), kwenye michuano ya ndani, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea Difaa El Jadida ya nchini humo, Simon Msuva havutiwi kabisa na matumizi ya teknolojia hiyo uwanjani.

Kwa mara ya kwanza Afrika, VAR ilianza kutumika kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) nchini Misri mwaka huu, kuanzia hatua ya robo fainali, lakini kama taifa kwa michuano yake ya ndani,

Morocco ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuanza kutumia teknolojia hiyo. VAR ilitumika kwa mara ya kwanza nchini Morocco kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Morocco Novemba 9, mwaka huu wakati Difaa El Jadida ikitolewa na TAS Casablanca kwa bao 1-0.

Bao hilo pekee lilipatikana kwa mkwaju wa penalti ambapo refa alilazimika kujiridhisha kwanza
kupitia VAR kabla ya kuizawadia tuta TAS Casablanca.

Hata hivyo, akizungumza na mwandishi wetu, Msuva alisema yeye haipendi kabisa VAR kwa sababu
inaondoa raha ya mchezo na kuwanyima nafasi mashabiki wa soka baadaye kubishana kuhusu
uhalisia wa mchezo.

"Kwanza inaondoa raha ya mchezo, lakini pia inawafuta wachambuzi wa soka kwani kila kitu tayari kinakuwa kimeshachambuliwa palepale, lakini kwa sababu ni teknolojia ambayo imeshakubalika mimi sina namna ya kuikataa," alisema Msuva.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad