Mchekeshaji, Idris Sultan ameripoti kituo cha polisi kati leo Novemba Mosi, 2019 na kuhojiwa na kutakiwa kuripoti tena Jumatano Novemba 6, 2019.
Jana asubuhi, Idris aliripoti kituoni hapo na kuhojiwa kwa saa tano na kupekuliwa nyumbani kwake, usiku aliachiwa kwa dhamana akitakiwa kuripoti tena leo saa 2 asubuhi, jambo ambalo amelitekeleza.
“Idris ameripoti kituoni saa 2:00 asubuhi na kuhojiwa kwa dakika 30. Wamechukua simu zake kwa uchunguzi na kutakiwa kuripoti tena Jumatano ijayo (Novemba 6, 2019).”
Wamemueleza kuwa kosa lake ni kusambaza habari za uongo chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao. Kosa la pili ni kujifanya Rais chini ya kifungu cha 15 cha makosa ya mtandao,” amesema, Benedict Ishabakaki ambaye ni mwanasheria wa mchekeshaji huyo.
Simu ya Idriss Yachukuliwa kwa Uchunguzi Akamatwa kwa Makosa Haya
0
November 01, 2019
Tags