Siogopi kuongeza idadi ya wanaonichukia - RC Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mamlaka zinakula rushwa, haiwezekani mtu analalamikiwa lakini bado anapewa kazi.

RC  Makonda kutokana na hilo amesema kuwa haogopi kuongeza idadi ya watu wanaomchukia.

Makonda alisema hayo katika ziara yake alipoingia kwenye mzozo na mkandarasi huyo ambaye alisema anafanya kazi kwa mujibu wa programu kama walivyokubaliana kitu ambacho kilionekana kumkera Makonda.

"Tanroads (viongozi wa Wakala wa Barabara) huyu Nyanza Road Works aliharibu mradi wa ujenzi barabara Temeke lakini mmempa tena kufanya mradi huu, kuna nini kinachoendelea?amehoji Makonda na kuongeza;

"Nasema mradi huu ndio wa mwisho. Sasa mumpe tena mradi mwingine mtanijua kama mimi ndio mkuu wa mkoa au nyie,"alisema na kumgeukia Ofisa Tawala wa Ilala, Jabiri Makame akimfokea.

Makonda alisema mkandarasi Nyanza Road Works ameharibu miradi mingi ikiwemo wa Nyakanazi kwenda Kakonko, Musoma na Temeke huku akishangaa kwa nini anaendelea kupewa miradi licha ya kuvurunda.

"Mamlaka zinakula rushwa, haiwezekani mtu analalamikiwa lakini bado anapewa kazi. Siogopi kuongeza idadi ya wanaonichukia, Nyanza Road Works tumempa zaidi ya sh milioni 800 lakini mpaka sasa anasuasua, vifaa hana ujanja ujanja tu,"amesema Makonda.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe ni baba masifa uchkiwe una kipi cha kufanya watu wakuchukie unajijua Mwenyewe unapenda kujipendekeza m

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad