Siri ya Meya wa CHADEMA Arusha kuhamia CCM


Aliyekuwa Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kupokelewa na Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.



Kalisti Lazaro ameyefika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, na ameeleza amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu akiwa katika Wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.

Kalisti amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Rais John Pombe Joseph Magufuli.

"Nimekuwa nikifanya kazi katika mazingira magumu nakutana na changamoto, nimeshletewa barua nyingi za onyo  kwa sababu ya kumsifia Rais, lakini pia siwezi kukaa chama ambacho kimejitoa kwenye Uchaguzi, leo Arusha inaenda kuwa ya CCM sababu wenzetu wamejitoa." amesema Meya Kalisti

"Nitaendelea kuwa Mwanasiasa kwa sababu niwaombe wananchi wa Kata yangu, nitaendelea kuwatumikia kwa nafasi nyingine ambayo chama changu itaamua mimi nirudi" ameongeza Meya Kalisti

Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMAa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad