Siri Yafichuka Kuhusu mfumo wa Oksijeni wa Ndege ya Boeing 787


Mfichua siri wa Boeing amedai kuwa abiria katika ndege ya 787 Dreamliner huenda wakaachwa bila hewa ya oksijeni ndege hiyo ikipata ghafla hitilafu ya kiufundi.

John Barnett anasema uchunguzi umebaini kuwa hadi robo ya mfumo wa oksijeni una hitilafu na kwamba huenda ikakosa kufanya itakapohitajika.

Pia anadai kuwa vipuri vya ndege vilivyo na kasoro vimewekwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikiundwa katika kiwanda cha Boeing.

Marekani kusuluhisha mgogoro wa mto Nile
Wanaume walio katika hatari ya kupata tezi dume
Boeing imepinga madai hayo ikisema kuwa ndege zake zote zinaundwa kwa kuzingatia viwango vy usalama vya hali ya juu.

Kampuni hiyo imejikuta mashakani siku za hivi karibuni baada ya ajali mbili mbaya zilizohusisha ndege yake ya 737 Max -iliyokuwa ya shirika la ndege la Ethiopia na kupata ajali mwezi Machi na ajali ya Lion Air ya Indonesia mwaka jana.

Bwana Barnett, ni injinia wa zamani wa udhibiti wa ubora, aliyefanya kazi na Boeing kwa miaka 32, hadi alipostaafu kwa misingi ya afya yake mwezi March mwaka 2017.

Kutoka mwaka 2010 aliajiriwa kama meneja anayesimamamia masuala ya ubora wa viwango vya uundaji ndege katika kiwanda cha Boeing cha North Charleston,Kusini mwa jimbo la Carolina.

John Barnett injinia wa zamani wa udhibiti wa ubora, katika shirika la Boeing
Kiwanda hicho ni moja ya viwanda vilivyohusika na uundaji wa 787 Dreamliner, inayotajwa kuwa ndege ya kisasa ya aina yake ambayo hutumika sana kwa safari ndefu kote duniani

Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa baada ya kuanza huduma zake ndege hiyo ilivutia mashirika kadhaa ya ndege kuimiliki, na imekuwa chanzo cha faidi kwa mashirika hayo.

Lakini kwa mujibu wa Bw. Barnett, 57, kinyang'anyiro cha ununuzi wa ndege hiyo mpya ilisababisha uundaji wake kuharakishwa, hali ambayo huenda ilifanya viwango vya usalama wake kutozingatiwa kikamilifu.

Shirika la Boing limepinga kauli hiyo na kusisitiza kuwa "usalama, ubora na uadilifu ni msingi wa utendakazi wa Boing".

Mashabiki wa Club Africain waichangia klabu yao mamilioni ya fedha
Mwaka 2016, anaiambia BBC, kuwa aligindua tatizo la kiufundi katika mfumo wa oksijeni ambayo inastahili kuwasaidia abiria na marubani kupata hewa endapo ndege itakumbwa na hitilafu ikiwa angani kutokana na sababu yoyote.

Mirija ya kupumulia hewa safi inatarajiwa kuning'inia kutoka juu ya ndege, ambayo inasaidia kupata hewa ya oksigeni.

Bila mfumo kama huo, abiria watashindwa kupumua. Ndege ikiwa inapaa umbali wa futi 35,000, kutoka ardhini au juu ya bahari abiria watazirai kwa chini ya dakika moja.

Ndege ikiwa inapaa umbali wa futi 40,000, hali hiyo inaweza kujitokeza katika kipindi cha sekunde 20. Wakati huo ubongo utaathiriwa na huenda abiria wakafariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad