Stars na Equatorial Guinea kukipiga Leo Taifa



ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Equatorial Guinea utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Stars inaingia kazini leo saa 1:00 usiku kurusha kete yake ya kwanza kwenye mchezo wa kufuzu Afcon inayotarajiwa kufanyika 2021 nchini Cameroon.

Ndayiragije amesema kila kitu kipo sawa kutokana na morali ya wachezaji kuwa kubwa.

"Wachezaji wana morali kubwa na wanatambua kazi yao ya kufanya kila mmoja atatimiza majukumu yake kikubwa ni sapoti ya mashabiki kujitokeza kwa wingi," amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad