Tamasha la Wasafi ''Wasafi Festival" Jijini Dar es Salaam Leo Sio Mchezo
0
November 09, 2019
Idea ya tamasha la wasafi lilianzia kupitia mashabiki wa Diamond kwenye group la WhatsApp linaloitwa Wasafi fans lenye members laki 5 ambao walitoa hiyo idea ya kwanini Wasafi wasiwe na tamasha lao likiwahusisha wasanii pekee wa label ya Wasafi tu.Hilo wazo likamfikia Diamond mwenyewe na akalifanyia kazi.
Mwaka 2016 ndo Wasafi wakaanza Hilo tamasha na likapokewa kwa ukubwa mkubwa na lilianza na mdhamini pekee alikuwa Vodacom na lilifanyika Dar, Iringa na Zanzibar.Mwaka 2017 alikufanyika kwa lengo la kuliboresha zaidi lakini pia huo mwaka Wasafi walikuwa na show nyingi Sana nje ya nchi so wakaamua hivyo.
Diamond akaona tamasha Hilo lisihusishe wasanii wa Wasafi pekee wakaona kuwe na wasanii wengine nje ya Wasafi na wakaanza kulifanya 2018 hapa wadhamini waliongeza kutoka mmoja kuwa wa5 ikiwemo Pepsi na hata jukwaa la kufanya tamasha wakalidesign katika namna tofauti na mwaka 2016 lakini pia waliongeza thamani kwa kuamua pia wafanye nje ya nchi wakafanya Kenya na Omani.
Tukija mwaka Huu wa 2019 tamasha hili likawa ni kubwa zaidi na mahitaji ya mashabiki kuongeza team nzima ya wasafi wakiongozwa na Diamond Platnumz a.k.a baba la wakaamua waongeze mikoa ya kufanya tamasha kutoka mikoa 6 kuwa 9 kwa kukua kwa tamasha la Wasafi imechangia wadhamini kuongezeka kutoka wa 5 kuwa 9 na hayo madhamini ni pamoja na Pepsi, Vodacom, Tanzania airway, startimes, Gsm mall,Tacaids na kampuni nyingine ndogo.
Leo Jumamosi ya tarehe 9 ndo wanaenda kuitimisha Wasafi festival Dar na ikiwa na wasanii karibia 30 au zaidi ikijumlisha wasanii wa bendi, hip-hop,taarabu na singer pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania Kama vile Wizkid, Tiwa Savage, InnosB na kijana mashashari anayekuja kwa kasi kwenye mziki wa East Africa Meddy kutoka Rwanda.Na good news Leo pia kampuni ya DSTV pia imeongezeka kwenye list ya wadhamini wa Wasafi Festival na kuwa mdhamini wa 10.
Tamasha la Wasafi limeteka headline blogs mbalimbali kutoka Ghana, Nigeria, Zambia, SA pamoja na East Africa wamekuwa wakireport show hii inaenda kufanyika kesho.Wasafi wameweka viingilio kuanzia 10,000, 50,000 na 500,000. Kwa kutambua ukubwa wa show ya kesho wametumia karibia wiki 4 kuweka stage iwe yenye ubora na pia walimleta design kutoka South Africa kwa ajili ya stage tu. Before ya show kutakiwa na mashindano ya kuimba na mshindi atakayepatikana atapata million 10 pia atapata bahati ya kufanya ngoma na msanii mkubwa wa wasafi Rayvanny boy a.k.a sauti ya vanilla na pia atasainiwa na label ya wasafi.
NB: kesho wasanii msituangushe mashabiki coz mtakuwa mnaangaliwa na watu wengi ndani na nje ya nchi so kazi ni kwenu
Tags