Tanzania yaporomoka viwango vya FIFA


Tanzania imeshuka kwa nafasi moja katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA hapoNovemba 28,2019, kutoka nafasi ya 133 na sasa inashika nafasi ya 134.

Kushuka kwa Tanzania kunajiri baada ya taifa hilo kupoteza 2-1 kwa Libya katia kundi J

Kwa upande mwingine Sare 1-1 dhidi ya Misri katika michuano ya kufuzu kwa kombe la mataifa mabingwa Afrika 2021 imeisaidia Kenya kupanda nafasi mbili juu katika orodha mpya za shirika hilo la kandanda duniani iliotolewa siku ya Alhamisi.

Katika orodha hiyo nayo Burundi ikishuka nafasi nane chini hadi nafasi ya 151.

Harambee Stars ya Kenya sasa ipo katika nafasi ya 106 duniani ikiwa ni nafasi mbili juu kutoka nafasi ya 108 ambayo ilikuwa ikishikilia wakati wa orodha ya miwsho iliofanyika Oktoba 24.

Timu hiyo ingepanda juu zaidi katika orodha hiyo iwapo wangepata matokeo mazuri dhidi ya Togo nyumbani katika mechi yao ya pili ya kufuzu.

Majirani Uganda hatahivyo wamepanda juu nafasi mbili zaidi hadi nafasi 77 na inasalia timu inayoorodheshwa juu zaidi huku Kenya ikiwa ya pili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad