Tanzia: Msanii Cheka Hija Mzee maarufu 'Bibi Cheka' afariki dunia


Aliyekuwa Msanii wa Muziki, Cheka Hija Mzee maarufu 'Bibi Cheka' amefariki dunia leo mchana Novemba 28 katika hospitali ya Mloganzila Mkoani Dar.

Kwa mujibu wa mtoto wa Msanii huyo mkongwe, aliyefahamika kwa jina la Adam Juma amesema mama yake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Bibi Cheka aliyekuwa chini ya Kundi la Wanaume TMK alipata umaarufu mkubwa kwa kuwa Mwanamuziki wa Kike mwenye umri mkubwa kuimba muziki wa Bongo Fleva.

Alipata umaarufu zaidi katika wimbo wake wa 'Ni Wewe' aliomshirikia Msanii kutoka Wanaume TMK, Temba lakini pia alishawahi kutoa wimbo na Msanii Marehemu Godzilla ulioitwa 'Good baba Fela'.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad