Tembo 115 wafariki kwa njaa Zimbabwe


Takriban tembo 115 wamefariki katika hifadhi kubwa ya wanyama nchini Zimbabwe tangu mwezi Septemba mwaka huu kutokana na uhaba wa chakula na maji.

Mnenaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi za Wanyama na Wanyamapori wa Zimbabwe (ZimPark), Tinashe Farawo alisema kuwa mabwawa ya maji yamekauka kwenye Hifadhi ya Hwange kufuatia ukame ambao umedumu kwa mwaka mzima.

Farawo alisema tembo 105 walikufa kati ya Septemba na Oktoba katika hifadhi kubwa ya wanyama,wakati wengine 10 walikufa tangu mwanzo wa mwezi huu. Alisema idadi ya vifo vilivyorekodiwa hadi sasa inaweza kuongezeka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad