T.I Aitolea Ufafanuzi Kauli Yake ya Kumcheki Mtoto Wake Bikira Kila Mwaka

Rapper T.I. amekaa na mkewe Tiny Harris pamoja na Jada Pinkett Smith kwenye "Red Table Talk" na kulitolea ufafanuzi suala lake lililoshika vichwa vya habari za dunia kwamba huwa anatabia ya kumpeleka binti yake Deyjah Harris kwa daktari wa wanawake kumuangalia kama bado ana usichana wake.

Alianza kwa kujisafisha kwamba watu walimuelewa vibaya

"Maana yangu ilitafsiriwa tofauti, acha niweke mambo sawa. Sikusema kwamba nilikuwa naingia naye kwenye chumba cha daktari. Hiyo ni kunitafsiri vibaya. Huo ni Uongo. Na pia sikusema Ä·wamba huwa ninafanya hilo kwa siku hizi, kwa sababu tayari ana umri wa miaka 18. Na sikusema Ä·wamba mama yake anakuwa hayupo, mama yake huwa anakuwepo na kila kitu." Ameeleza T.I.

Licha ya yote, alimuomba radhi binti yake Deyjah na pia aliweka wazi kuwa alikuwa anafanya vile wakati binti yake huyo akiwa na umri wa miaka 15 na 16 lakini kwa sasa haipo tena hivyo.

Kama utakumbuka mahojiano yale ya T.I. na Podcast ya "Ladies Like Us" ya Nazanin Mandi na Nadia Mohan yaliyoibua sakata hili yalifutwa mtandaoni lakini athari ilikuwa kubwa hadi kupelekea Deyjah kum-unfollow baba yake mzazi na hata pia baadaye kuzifuta akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad