Tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi - IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro amezungumzia suala la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kupigwa risasi ambapo amesema mpaka sasa bado hawajambaini mtu aliyefanya tukio hilo, huku akieleza kwamba Tundu Lissu ameshindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo jambo ambalo linachukua muda.

Ameeleza hayo katika kipindi maalum cha Konani kinachorushwa na ITV kupitia Mitandao yake ya kijamii ambapo wamesema kwa sasa wanangojea kurejea kwa Lissu ili afungue kesi.

"Sisi tunamsubiri Mhe. Tundu Lissu aje afungue kesi, kitu gani kimemtokea, mazingira gani na yule dereva wake, dereva tumemtafuta imekuwa shida, yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao" amesema IGP Sirro.

IGP Sirro ameweka bayana kwamba kesi ya jinai mara nyingi haifi hata ikichukua miaka kumi bado ni kesi ya jinai.

"Kimsingi ni kwamba kesi ipo tunamsubiri Bwana Lissu aje atupe taarifa ilikuwaje na yule shahidi yake nafikiri tutapata sehemu ya kuanzia," amesema.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sirro, Tundu si Mh tena.
    kwa taarifa yako amesha vuliwa Uheshimiwa baada ya Uchaguzina kupatikana mshindi wa kuwawakilisha wana Singida Mashariki.

    Hhuyu msaliti Haludigi, Je ulaia wake niwa kielektoniki..?

    ReplyDelete
  2. Sirro, Tundu si Mh tena.
    kwa taarifa yako amesha vuliwa Uheshimiwa baada ya Uchaguzina kupatikana mshindi wa kuwawakilisha wana Singida Mashariki.

    Hhuyu msaliti Haludigi, Je ulaia wake niwa kielektoniki..?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad