Urusi yashika uwanja wa ndege Syria

Urusi imetangaza leo kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege uliotelekezwa mapema wiki hii na vikosi vya jeshi la Marekani kaskazini mwa Syria.

Shirika la habari la Urusi (TASS) limemnukuu ofisa mmoja wa ngazi ya juu akisema wanajeshi wa nchi hiyo wanashika doria kwenye uwanja huo wa ndege karibu na mji wa Kobane karibu mpaka wa Uturuki.

Urusi imesema Marekani iliutumia uwanja huo kuviunga mkono vikosi vya wapiganaji wa upinzani kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Wakati huohuo Rais wa Syria, Bashar al-Assad amesema katika mahojiano na sauti ya Ujerumani kwamba kuwapo kwa Marekani nchini Syria kutasababisha upinzani wa kijeshi ambao utavilazimisha vikosi vya nchi hiyo yenye nguvu kubwa za kijeshi kuondoka nchini humo.

Marekani ilitangaza wiki hii kubakisha kikosi cha wanajeshi 600 nchini Syria ili kupambana dhidi ya kundi linalojiita dola la Kiislamu (IS).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad