Viongozi Vyama vya Upinzani hawana ushirikiano


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali, inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa vijana na wanawake, ikiwemo masuala ya upigaji wa kura, Elvis John, amesema kuwa viongozi wa ngazi za juu kutoka vyama vya upinzani, hawana ushirikiano wala mahusiano ya ukaribu na wagombea wa
 ngazi za chini, hali iliyopelekea wagombea wengi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa majina yao kuenguliwa.

Hayo ameyabainisha leo Novemba 28, 2019, wakati wakitoa tathmini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ambapo amesema kuwa kutokuwepo kwa mahusiano mazuri ya viongozi hao na wagombea, ilipelekea wagombea wengi katika uchaguzi huo kujijazia fomu wenyewe, bila ya kupewa muongozo wala maelekezo yoyote kutoka ngazi za juu.

"Tulikuwa na kibali cha uangalizi wa uchaguzi huo kutoka TAMISEMI, ile idadi kubwa ya watu ambao majina yao yalienguliwa wengi wao walikuwa wanafanya makosa madogo katika ujazaji wa fomu, wanachama wengi wa vyama vya siasa hawana mahusiano na viongozi wao wa juu wa vyama, hata vyama vilipoamua kujitoa kuna baadhi ya wagombea hawakupenda hiko kitu unakuta wananung'unika tu kwa vile Mwenyekiti wa chama keshaongea" amesema Mkurugenzi Mtendaji wa TAFEYOKO.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulifanyika Novemba 24, 2019, ambapo Chama cha Mapinduzi kiliibuka kidedea kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 90, huku vyama vya siasa vya upinzani, vikijitoa katika kinyang'anyiro hicho kwa kile walichokieleza kuwa hawakutendewa haki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad