Viongozi wa vyama vya Ushirika watakiwa kutotumia fedha za wanachama bila idhini ya Mkutano mkuu wa Chama.


SALVATORY NTANDU
Viongozi wa Chama cha  Ushirika wa  akiba na mikopo SHIRIKISHO SACCOS LIMITED wilayani  Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutotumia fedha za wanachama kinyume na makisio yalioridhiwa  na mkutano mkuu na badala yake ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija.

Hayo yamebainishwa na Daniel Kimatha na Prisca Agustino kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa SHIRIKISHO SACOSS LIMITED uliofanyika Mjini kahama ambao ulikuwa na lengo la kutathimini hoja mbalimbali zinazokikabili chama hicho kwa mwaka 2019 na kuangalia namana bora ya kuzipatia ufumbuzi.

Wamesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongzo katika shirikisho hilo kutumia fedha kinyume na makisio yaliyoridhiwa na mkutano mkuu wa mwaka na kusababisha kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wanachama wao na badala yake wanapaswa kuwashirikisha kabla ya kufanya matumizi.

“katika mwaka huu wa 2019 viongozi wetu wametumia shilingi laki mmoja kinyume na makisio yalioridhiwa na mkutano mkuu suala hili halikubaliki walipaswa kutushirikisha,alisema Kimatha.

Akijibu hoja hizo Mwenyekiti wa {SHIRIKISHO SACCOS LIMITED} Tito  Greyson Okuku amekiri kujitokeza kwa suala hilo na kusema kuwa walitumia fedha za faida walizopata kutokana na rida walizokusanya  na kuomba radhi wanachama hao na kuahidi kuwa suala hilo halitajitokeza tena.

Kwa upande Dronick Kamugisha ni afisa Ushirika wa Halamshauri ya Mji wa Kahama amesema kutokana na kasoro mbalilimbali zilizojitokwza katika chama hicho wao kama Halamshauri wamejipanga kutoa elimu ili wananchama waelewe dhima ya Ushirika na namna bora ya Uendeshaji.

Naye Mkaguzi wa vyamba vya Ushirika mkoa wa Shinyanga Rodrick Kilemile  amesema ofisi yake imebaini vyama vingi vya ushirika hawana wataalamu wa mahesabu hali ambayo imekuwa ikiwapa shida katika uandaaji wa taarifa za mwaka na kusababisha kuwepo kwa migororo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad