Wagombea Wote wa Upinzani Waliopitishwa Kugombea Nachingwea wajitoa


Na Ahmad Mmow-Nachingwea

Wanachama wa vyama vya upinzani ambao waliteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wilayani Nachingwea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 wamejitoa kushiriki katika uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea, Nnunduma Ali alipozungumza na Muungwana Blog, leo mjini Nachingwea.

Nnunduma alisema wagombea wa nafasi  mbalimbali walioteuliwa kutoka vyama vya CHADEMA na CUF wamejitoa wenyewe kwa kuandika barua, pia ngazi za vyama zilizowadhamini viliandika barua za kujitoa.

 ''Hadi kufikia tarehe 16.11.2016, jioni wagombea wote waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali  kupitia vyama vya CUF na CHADEMA walikuwa wamejitoa. Sisi kama wilaya tunaandaa fomu za matokeo zitakazotumika kuwatangaza viongozi hao, tutabandika kwenye mbao za matangazo siku ya tarehe 24.11.2019,'' alisema Nnunduma.

Msimamizi huyo wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea alisema awali Chama cha Mapinduzi asilimia 98 ya wanachama wake waligombea nafasi mbalimbali walipita bila kupingwa, kwahiyo baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa ni dhahiri kimeshinda kwa asilimia mia moja.

Nnunduma aliitaja idadi ya viti vilivyotarajiwa kugombewa ni vijiji 127, vitongoji 525, viti maalumu vyote 997 na viti mchanganyiko 1556. Wakati vyama vilivyosimamisha wagombea vilikuwa CUF, CHADEMA na CCM. Akivitaja vyama ambavyo wagombea wake walichukua fomu na kurejesha ni CUF, CHADEMA, ADC na CCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad