Wakati mwingine wadada sijui mnataka mfanyie nini ili mjue kuwa hamtakiwi! Mwanaume hajakuoa, anakupiga kila siku, kila siku anabadilisha wanawake, sio kwa kificho, hapana, anawaleta mpaka ndani? Yaani unajua na ukiuliza anakupiga. Unabeba mimba yake, anakufukuza na mimba yako au anaacha kuhudumia mtoto.
Unaanza kulalamika kuwa umetelekezwa, dada yangu mwanaume alishakuacha muda mrefu, alishakuambia hakutaki tena kwa matendo, ulitegemea nini? Wakati mwingine jiongze mwenyewe! Mnajiambia “Alisema atabadilika!” Dada yangu mwanaume hasemi niabadilika, anabadilika, sasa wewe ni mtu mzima, una akili zako, mtu anakupiga mpaka unazimia unataka abadilike nini?
Unajua mlalamaika kuwa hampendwi wakati hata nyie wenyewe hamjipendi? Mwanaume anakuambia sikutaki, anakupiga, mwingine anapigwa mpaka unalazwa ho9spitalini halafu bado unamng’ang’ania, hivi unajipenda kweli wewe? Halafu unataka akuoe akuleleke wapi? Kwa anayokufanyia ndoa si inamaana unapelekwa Mochwari moja kwa moja, Dada ishu sio kama anakupenda au hakupendi ishu ni je wewe unajipenda?
Kama wewe hujipendi, hutambui thamani yako basi jua ni ngumu kupendwa! Najua kuna ambao mpo kwenye ndoa na hamuezi kutoka, lakini hujaingia kwenye ndoa, ni mpenzi tu anakupiga mpaka unalazwa hivi na wewe unang’ang’ania nini? Unabana na pua kabisa “Aliniambia kuwa atabadilika!” Hivi una akili kweli, kwahiyo siku akija akikuambia Baba yake ni Obama utakubali kwakua wakati anakuambia alikua analia au aliwaita na ndugu zake!
Hembu anza kujipenda wewe kwanza, anza kwa kujionea huruma, jiambie “Nitakufa!” kisha jifanyi ekitu hata kimoja ambacho kinakupa raha, yaani kama ni mpare Pika Makande yako unga na nazi kula na parachihi sikia raha kana kwamba hakuna kesho. Anza na vitu vidogo vidogo utaona mambo yaanabdilika, soma kitabu changu sehemu ya nne kisha jipende uone utapendwa mpaka na mbuzi, sio mtu unajichukia mpaka Inzi wanakukimbia!