'Waliotoweka Mtwara ni wahalifu' - RPC Mtwara

Kamishina Msaidizi wa Polisi mkoani Mtwara, ACP Blasius Chatanda, amesema kuwa jumla ya watoto 11 waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha, kutoka katika kijiji cha Mtimbwilimbwi, Halmashauri ya Nanyamba, huenda wakawa wameenda nchini Msumbiji


kwa ajili ya kujiunga na vikundi vya uhalifu, kama ambavyo awali walikuwa.

Akizungumza na EATV &EA Radio Digital, leo Oktoba 31, 2019, ACP Chatanda amesema kuwa kulingana na historia iliyopo juu ya watoto hao ya kuwa waliwahi kukamatwa na maafisa wa usalama nchini Msumbiji kwa makosa ya uhalifu na kurejeshwa nchini, huenda hata sasa wakawa wameenda kujiunga na vikundi hivyo tena.

"Hawa watoto waliwahi kuingia kwenye makundi ya uanaharakati nchini Msumbiji, wakakamatwa na kurejeshwa, wako watu wengine wazima hapo Kijijini wameondoka ambao tunaamini hao ndiyo walikuwa kiungo na wameacha familia zao, tunaamini huenda hawa nao wameendoka nao, sio kwamba wametekwa ama kuuawa, tunaamini wamerudi huko huko Msumbiji, ambako mwanzo walikamatwa na kurudishwa" amesema ACP Chatanda.

Watoto hao 11 wanadaiwa kutoweka wote kwa pamoja, kati ya Oktoba 10 na 15, 2019, na kwamba Jeshi la polisi mkoani humo, linafanya mawasiliano na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Msumbiji ili kuangalia namna ya kuwapata na kuwarejesha nchini.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad