Wanachama Sita wa CHADEMA watupwa rumande kwa tuhuma za kuvunja na kuiba


Wafuasi Sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Njombe wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Njombe kwa tuhuma za kuvunja, kuiba na kuharibu mali za chama cha mapinduzi katika kijiji cha Ibiki kilichopo kata ya Igongolo wilayani Njombe

Akitaja kwa mara kwanza kesi hiyo nambari 179 hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe James Mhanusi  amesema watuhumiwa wote sita ambao ni Asifiwe Muhoka, Lupyana Mtimbuka , Baraka Mkula, Casimil Chongolo, Jacob Ngimbudzi na Gaston Mhiche,  Novemba 20 walivunja,kuiba na kuharibu mali za chama cha mapinduzi katika ofisi iliyopo kijijini hapo kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha sheria no 296(a)(b) cha penal Code cha 2002.

Watuhimiwa wamerudishwa lumande mpaka pale kesi itakapo tajwa tena Disemba 4 mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad