Wananchi Waonywa Juu ya Wizi wa Taa za Barabarani


Na Theo Mwambasi George, Kigoma.

Wananchi wa Kata ya Kigoma mjini Mkoani Kigoma wametakiwa kuonesha ushirikiano katika kuzuia na kutokomeza wizi wataa za barabarani ambazo zimewekwa katika barabara mbalimbali za mitaa.

Akizungumza na Muungwana Blog hii leo katika ofisi ya Meya wa Kigoma Diwani Husein Kalyango amesema kuwa licha ya kutangaza kuwa raia yeyote atakaetoa taarifa juu ya wizi wataa hizo atapewa fedha lakini kwa bahati mbaya ushirikiano wa wananchi wake umekosekana licha ya kuwa taa zinaibwa kila mara.



Aidha Kalyango amesema kuwa Zaidi ya taa 100 zimeibwa katika maeneo mbalimbali ya mitaa ikiwemo Mjimwema,mwanga ambazo kuanzia mwaka jana 2018 sola za taa na betri zimekuwa zikiibwa katika maeneo hayo licha ya kuwa taa hizo zipo kwaa ajili ya kupunguza giza katika mitaa.

Pia amesema kuwa ni aibu kwa mdhamini kuona anadhamini taa kisha zinaibwa na wananchi wasio waaminifu hivyo kupelekea bajeti kubadilika kwani taa hizo ni gharama kubwa.



Hivyo ametoa wito kwa jamii kulinda miundo mbinu ya umma kwani wizi sio mzuri kwani hupelekea baadhi ya mwananchi kuchukua sheria mkoni kama ilivyo tokea mwasenga ambapo kijana alietaka kuiba taa akakamatwa na kuuliwa .

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad