'Wanaombeza Rais ni wafuasi wa Shetani' - Lugola


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kuna kikundi cha watu wachache ambao wanabeza maendeleo yanayofanywa na Rais John Pombe Magufuli na kumuomba Rais Magufuli asikate tamaa, aendelee kufanya kazi.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa nyumba za Polisi, zoezi ambalo lilifanywa na Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro.

"Wachache ndiyo wanaobeza jitihada za Rais hata kwenye kiganja hawajai, tena ni wafuasi wa ibirisi shetani, niwaambie Rais anaitegemea 'Isaya 41', inayosema utawapepeta na upepo wa kisulisuli, Rais usiogope wanaokubeza watapeperushwa" amesema Waziri Lugola.

Awali IGP Sirro amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa kwenye zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajia kufanyika hivi karibuni utaenda kwa amani na usalama.

"Rais nikuhakishie uchaguzi uliopo mbele yetu utafanyika kwa amani na tumejipanga" amesema IGP Sirro.


CURRENT AFFAIRS
CHADEMA yatoa maagizo matatu kuhusu Halima Mdee

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lugola nafikiri hawataki naendelea ya ya nchi nzima, Bali maendeleo yao binafsi na watoto wao na wale wawapendao tu, na wanayataka ikibidi kwa gharama yoyote Ile ikibidi hata kuiuza nchi au kuifilisi kabisa ili mradi tu wao na jamaa zao wameshiba

    ReplyDelete
  2. Hawa ni Mabahalia wanaeleweka Ni Wazamiaji kutoka Nchini Twita na Flashi
    zaoMifukoni..Ninjaaa WAPEKENYUEEEEE.

    ReplyDelete
  3. Hawa ni Mabahalia wanaeleweka Ni Wazamiaji kutoka Nchini Twita na Flashi
    zao Mifukoni..Wengine Memori zimejaa na wengine Mafaili kichwani yameshakuwa koraptedi wanaomba usaidizi toka nchi ya jilani zao Fesiuku,... Ninjaaa WAPEKENYUEEEEE.

    ReplyDelete
  4. Hawa ni Mabahalia wanaeleweka Ni Wazamiaji kutoka Nchini Twita na Flashi
    zao Mifukoni..Wengine Memori zimejaa na wengine Mafaili kichwani yameshakuwa koraptedi wanaomba usaidizi toka nchi ya jilani zao Fesiuku,... Ninjaaa WAPEKENYUEEEEE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad