KENYA:
Maafisa nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na matukio ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo la Pokot Magharibi imefikia 37
Maporomoko hayo yaliathiri zaidi Vijiji vya Nyarkulian na Parua ambapo pia daraja linalounganisha Vijiji hivyo limeharibiwa kabisa na hivyo kutengenisha Vijiji hivyo
Aidha, maafisa wa Uokoaji wamesema kuwa miili ya watu 12, ikiwemo ya watoto 7 imepatikana asubuhi ya Jumamosi huku Kamishna wa Jimbo hilo, Apollo Okelo akisema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na shughuli za uokoaji zinaendelea
Huku picha zikionesha miti na miundombinu mingi kuharibiwa Kamishna huyo ameainisha kuwa, "Tunajaribu kutafuta mahali ambapo daraja limesombwa na maji ya mafuriko.”