Watu 6 Wafikishwa Mahakamani na TAKUKURU Kwa Uhujumu Uchumi


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jumatano Novemba 20, imewakamata na kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara sita wakiwamo raia wa kigeni kutoka nchini China kujibu mashtaka ya Rushwa na uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi), Wli Mfuru amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani kuwa ni You Hattao, Zhang Zhi Xin wote raia wa China, wengine ni John Mnyele, Loncolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro, ambao wote ni watanzania.

Amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakimiliki kampuni maeneo ya Kibaha inayotengeneza na kuuza mafuta aina ya Dizeli yaliyo chini ya kiwango na kuyauzia baadhi ya kampuni zinazofanya biashara hiyo bila kufuata taratibu za ufanyaji biashara.

"Uchunguzi uliofanywa na Takukuru kwa kushirikiana na jeshi la polisi limebaini kampuni ya SHIN UP iliyopo Visiga imejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja  na uhujumu uchumi na kusababisha serikali hasara ya zaidi ya 1.2 bilioni," amesema Mfuru

"Pamoja na mambo mengine, kampuni hii imeghushi vyeti vya kuwawezesha kufanya biashara nchini, inakwepa kodi pamoja na watuhumiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu," alisema

Amewataja watuhumiwa hao ni Yu Hattao na Zhang Zhi ambao wote ni raia wa China, John Mnyele, Lincolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro ambao ni Watanzania.

Mfuru amesema Oktoba 3O, 2019 Takukuru iliwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu kati ya hao ambapo washtakiwa wengine wameeunganishwa nakuongezewa mashtaka yakiwemo utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad