Watuhumiwa Wizi Komputa za DPP Wameachiwa, Tunampeleza Idris”


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amekiri kuwa washukiwa wa wizi wa Computer za ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Wameachiwa kwa dhamana na hawajawafikisha Mahakamani kwa kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa wao kuhusika na uwizi huo.



Aidha, Kamanda Mambosasa amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi juu ya shitaka la jinai linalomkabili mchekeshaji Idris Sultan.



Mambosasa ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar, leo Ijumaa, Novemba 22, 2019; “Jeshi la Polisi linafanya upelelezi sio kila kosa linakwenda Mahakamani.”



“Kulikuwa na taarifa za hujuma kwenye ofisi za serikali za vyama na hata za maeneo mengine kimsingi yanatakiwa kuwa salama, kulikuwa na taarifa kuwa kuna watu wanajipanga kwa ajili ya kuendesha vitendo vya kihalifu kwa hujuma za kauribu miundombinu.



“Novemba tarehe 24/11/2019 ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa,hivyo basi sisi Jeshi la Polisi tutaimarisha ulinzi maeneo yote ya Dar es Salaam,nimeomba Askari 1000 kutoka vikosi vingine hili niweze kuimarisha ulinzi. Katika uchaguzi huo sisi kama Jeshi la Polisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba hali ya amani, utulivu na usalama inaimarishwa kwa kiwanga cha asilimia ya juu.



“Hatutaishia hapo tumejipanga kuhakikisha kwamba tunatumia wadau wote ndani ya kambi kuhakikisha zoezi hili linakwenda salama, nafahamu sehemu zitakazofanya uchaguzi zitakuwa chache lakini Jeshi la Polisi litakuwa kila sehemu.



“Tutahakikisha kwamba sehemu ambazo zinafanya uchaguzi zinakuwa salama na sehemu ambazo wahusika wamepita bila kupigwa zinaendelea kuwa salama, ulinzi wetu unalenga kuhakikisha raia na mali zao wanakuwa salama,”



“Ofisi za vyama vyote vya siasa zinaendelea kuwa salama lakini mali za watanzania ndani ya kanda zinaendelea kuwa salama pia.



“Juzi Rais akiwa Morogoro kuna mtu alijitambulisha, mimi mpiga debe yani ndiyo kazi yake lakini mliona maelekezo aliyo yatoa Rais upigaji wa debe ni marufuku, kondakta anaruhusiwa anatosha kumfanya abiria akapokelewa na kusafiri”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad