Waziri Jafo akemea viongozi wanaotoa matamko ya kuhatarisha amani

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekemea wadau wa siasa wanaotoa matamko ya kuhatarisha amani katika kipindi hiki ambacho chaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utahitimishwa Tarehe 24/11/2019.

Mhe. Jafo ameyasema hayo Mkoani Njombe alipokua akizungumza na kamati ya Ulinzi na usalama, kamati ya rufaa na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe. 
                 
Alisema baadhi ya wadau wa siasa wanatoa matamko ya kuhatarisha amani ya Nchi sidhani kama ni busara kutamkia Nchi yako maneno mabaya ya kukatisha tamaa, kuvunja mioyo na kutishia amani ingependeza zaidi kama kila mmoja wetu angetekeleza jukumu lake la kisiasa na wakati huo huo kulinda amani ya Nchi.

“Kama mtu anaona ameonewa katika mchakato wowote wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kamati za Rufaa zipo apeleke malalamiko yake huko akiona hayajashughulikiwa ndipo anaweza kutoa lawama:

Cha ajabu ni kuwa watu hawajapeleka malalamiko yao kwenye Kamati ya Rufaa wanalalamika maeneo ambayo si stahiki hivi hawajitendei hako maana Kanuni imeelekeza wapi pa kwenda endapo umeona umedhulumiwa haki yako” alisema Jafo.

Kama watu wameenguliwa kwenye kinyang’anyiro wanastahili waende kwenye Kamati ya Rufaa waone kama malalamiko yao yatashughulikia au lah; nashauri wadau wote wa siasa kufuata Kanuni za Uchaguzi ili zoezi likamilike kwa amani.

Halkadhalika Mhe. Jafo alizitaka Kamati za Rufaa kuhakikisha wanawatendea haki wale wote watakaowasilisha malalamiko yao kwenye Kamati hizo.

“Huu Ndio muda  pekee  wa Kamati ya Rufaa   kuonyesha umahiri wenu katika zoezi hili na kuweka sawa mambo yote ambayo hayakwenda sawa na kusababisha malalamiko”

Aliongeza kuwa Kamati za Rufaa msibanwe na chama chochote wala maelekezo ya aina yeyote fanyeni kazi hii kwa misingi ya sheria iliyowekwa tendeni haki stahiki kwa kila mlalamikaji hatimaye mpate ufumbuzi wa malalamiko yote yatakayowasilishwa aliongeza Jafo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad