Waziri Mbarawa Afuta Mamlaka Za Maji 36


Katibu mkuu wizara ya Maji Profesa Kilila Mkumbo,amesema serikali imefuta mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 36 na sasa zitahudumiwa na mamlaka za makao makuu ya mikoa 25, zilizoundwa na kuongezewa majukumu ya utoaji huduma katika maeneo yake

Hayo ameyasema jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Wizara juu ya maboresho ya muundo mpya wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini.

Prof.Mkumbo,amesema kuwa katika kuimarisha uendesahiji wa sekta ya usambazaji maji na usafi wa mazingira mijini, Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa, kwa mamalaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria ameongeza maeneo ya huduma za maji.

“Kwa mujibu wa sheria ya huduma za maji na iusafi wa mazingira Na 5, ya mwaka 2019 ameongeza maeneo ya huduma kwa baaadhi ya mamalaka za maji na usafi wa mazingira nchini aidha Waziri wa maji ameanzisha na kufuta baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini”amesema Prof.Mkumbo

Hata hivyo amesema kuwa kwenye mabadiliko hayo kutakuwa na mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 25, katika ngazi ya makao makuu au miji mikuu ya mikoa.

Hata hivyo ameongeza kusema kuwa mamlaka hizo zitahudumia halmashauri zilizopo katika miji mikuu,makao na makuu ya mikoa husika.

“Aidha baadhi ya mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira katika ngazi hii zimeongezewa maeneo ya huduma na kuunganishwa na baadhi ya miji midogo katika mikoa husika au mikoa ya jirani,”amesisitiza

Prof.Mkumbo amezitaja baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira za mikoa zilizoongezewa majukumu kuwa ni pamoja na mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Dar es saalam (DAWASA) ambayo itahudumia hadi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga.

Nyingine ni Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma (DUWASA), ambayo nayo pia itahudumia eneo lake la jiji pamoja na miji ya Kongwa, Bahi na Chamwino

Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mrogoro (MORUWASA) ambayo imeongezewa miji ya Kilosa na Mikumi.

Nyingine ni Mamalaka ya maji na usafi wa mazingira ya Mwanza (MWAUWASA) ambayo itahudumia halmashauri ya jiji la Mwanaza na manispaa zake na mji wa Magu, Nansio na Ngudu

Hata hivyo amesema kuwa Vmamalaka za maji na usafi wa mazingira za miji midogo ya wilaya 40, zitasimamiwa na mamlaka ya maji vijijini (RUWASA).

Baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira zilizofutwa kati ya 36, ni pamoja na Kibaha WSSA, Kongwa WSSA, Chamwino WSSA, Kilosa, Kyela WSSA, Mikumi WSSA, Pangani WSSA, Magugu WSSA.

Amesema kuwa lengo la Serikali kufanya hivyo ni kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya fedha .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad