Waziri Mkuu aagiza nyumba za Kigamboni zijengwe
0
November 28, 2019
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma katika Wilaya Kigamboni, jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika haraka ili ziuzwe au kupangishwa kama ilivyokusudiwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni.
Waziri Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba nyingi nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze kukamilika.
Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba zake 161 zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.
Ili kufanikisha jambo hilo Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.
Pia, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwasaidia watumishi wa Wilaya na Halmashauri hiyo kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.
Tags